11 Oktoba 2020

               Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com         EIN: 82-5217331

Jumapili 2:00 – 4:00                                                                    11 Oktoba 2020

Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;
nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944

4 Oktoba 2020

     

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com         EIN: 82-5217331

   KARIBU TUJIFUNZE NENO LA MUNGU KWENYE KANISA

                                                              LA

                  SWAHILI  EVANGELICAL  LILIPO GEORGIA ATLANTA.

                                                     OCT.04th  – 2020

THEME: TABIA NNE ZA KIMWILI ZA WATU WASUMBUAO KANISA LA KRISTO.

ANDIKO : WARUMI. 8:8Wale waufuatao Mwili awawezi kumpendeza Mungu”

NASABA FUPI YA KITABU CHA WARUMI:

Kwa ufupi waraka huu uliandikwa na Paulo Mtume kwa mataifa mnamo mwaka wa 57 AD, pale  Korintho, Nyaraka hii iliandikwa wakati Paulo akijiandaa kwenda Jerusalemu.

Lengo la kitabu hiki :

1. Lengo kubwa kabisa ilikuwa nikuwaonya wakristo  na Kanisa lilioko Rumi ili wawe na Imani ya kweli katika Kristo Yesu,

2. Ilikuwa ni kujitambulisha kwake, kwa wakristo walioko Rumi kabla ya yeye kufika pale Rumi.

            Tujifunze kuhusu Tabia nne za watu wanao tesa Kanisa la Kristo.

Tabia #:01. WATU WENYE ROHO YA WIVU.( Watu wa Kimwili)“Rom.8:8” “ Mwaz.3:3 ”

 Asili ya wivu ni shetani.

Tabia #:02. WATU WA  KIBURI  na MAJIVUNO (watu wakimwili) “Mith. 8:13, Luk.1:51”

Mfano: Maisha ya watu Hapa Marekani.

Tabia #: 03. Roho ya Kupenda Vyeo Visivyo kukustahili na kutotii mamlaka yaliyopo,

                                          (viongozi wa kimwili) “Roma.13:1-3”

Tabia #: 04. Watu wasio Tii Neno la Mungu. “ Rom.2:8,”

                                                                                –  Awataki Maombi,

                                                                                –  Awataki kujifunza Neno la Mungu,

                                                                                –  Watu watabia zote za dhambi.

Watu wa Tabia hizo hukumu kubwa ya kutisha inawasubiri na wote watatupwa kwenye ziwa la moto.”Ebr.10:27”.

NB: Kwaiyo inatupasa tuache tabia zote za kimwili na tumfanyiye Mungu kazi kwa Upendo, Amani, Ushirika Mtakatifu. “Yak.4:7”

Inawezekana maisha yako yako hatarini pasipo kufahamu, umetenda dhambi pasipo kujuwa lakini pia Unaishi maisha ya kulazimishwa kidhambi, Naomba uje tuombe Pamoja na wewe.

                                          Mbarikiwe Nyote na Kristo Bwana Wetu.

                                      By Pastor. Mokwa Ferdinand John.

                                                                             AMEN.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944

27 Septemba 2020

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com         EIN: 82-5217331

Jumapili 2:00 – 4:00                                                                    27 Septemba 2020

Waebrania 2: 3 – 4

sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;
Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.

Yohana 5: 8 – 11

Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.
10 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro.
11 Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende.

Yohana 9: 13 – 16

13 Basi wakampeleka kwa Mafarisayo yule aliyekuwa kipofu zamani.
14 Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya zile tope na kumfumbua macho.
15 Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona.
16 Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa matengano kati yao.

Yohana 11: 43 – 50

43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.
44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
45 Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini.
46 Lakini wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu.
47 Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.
48 Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu.
49 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote;
50 wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima.

Yohana 20: 30 – 31

30 Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki.
31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021 (641) 990-7245             (404) 587-0944

20 Septemba 2020

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com         EIN: 82-5217331

Jumapili 2:00 – 4:00                                                                     20 Septemba 2020

Yohana 2: 1 – 11

Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.
Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.
Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.
Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.
Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni.
Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.
Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.
Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.
Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,
10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.
11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

Yohana 4: 46 – 54

46 Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu.
47 Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani.
48 Basi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa?
49 Yule diwani akamwambia, Bwana, ushuke asijakufa mtoto wangu.
50 Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia.
51 Hata alipokuwa akishuka, watumwa wake walimlaki, wakisema ya kwamba mtoto wake yu hai.
52 Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa hajambo; nao wakamwambia, Jana, saa saba, homa ilimwacha.
53 Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake.
54 Hiyo ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu, alipokuwa ametoka Uyahudi kufika Galilaya.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944

6 Septemba 2020

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com          EIN: 82-5217331

Jumapili 2:00 – 4:00                                                                        6 Septemba 2020

Matendo Ya Mitume 2: 14 – 21

14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.
15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;
16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.
19 Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi.
20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.
21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944