24 Januari 2021

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com         EIN: 82-5217331

Jumapili 3:30 – 5:30                                                                                    24 Januari 2021

Kutoka 16: 2 – 9

Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung’unikia Musa na Haruni, huko barani;
wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa Bwana katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote.
Ndipo Bwana akamwambia Musa, Tazama, mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mkate kutoka mbinguni; na hao watu watatoka nje na kuokota kila siku sehemu ya siku; ili nipate kuwajaribu, kwamba watakwenda katika sheria yangu, ama sivyo.
Kisha itakuwa siku ya sita, ya kwamba watayaandaa hayo watakayoleta ndani, nayo yatakuwa ni mara mbili kuliko wayaokotayo kila siku.
Musa na Haruni wakawaambia wana wote wa Israeli, Jioni ndipo mtakapojua ya kuwa Bwana amewaleta kutoka nchi ya Misri;
na asubuhi ndipo mtakapouona utukufu wa Bwana; kwa kuwa yeye asikia manung’uniko yenu mliyomnung’unikia Bwana; na sisi tu nani, hata mkatunung’unikia?
Musa akasema, Ndilo litakalokuwa, hapo Bwana atakapowapa nyama wakati wa jioni mle, na asubuhi mikate hata mkakinai; kwa kuwa Bwana asikia manung’uniko yenu mliyomnung’unikia yeye; na sisi tu nani? Manung’uniko yenu hayakuwa juu yetu sisi, ila juu ya Bwana.
Musa akamwambia Haruni, Haya, sema na mkutano wote wa wana wa Israeli, Njoni karibu mbele ya Bwana; kwa kuwa yeye ameyasikia manung’uniko yenu.

Waefeso 4: 29

29 Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

Warumi 1: 28 – 31

28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;

Warumi 12: 2 – 3

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944

13 Decemba 2020

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com         EIN: 82-5217331

Jumapili 3:30 – 5:30                                                                                     13 Desemba 2020

Isaya 53: 1 – 12

Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?
Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.
10 Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake;
11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.
12 Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944

8 Novemba 2020

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com         EIN: 82-5217331

Jumapili 2:00 – 4:00                                                                      8 Novemba 2020

Luka 5: 1 – 10

Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,
akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao.
Akaingia katika chombo kimoja, ndicho chake Simoni, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.
Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.
Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;
wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama.
Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.
Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata;
10 na kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni. Yesu akamwambia Simoni, Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944

11 Oktoba 2020

               Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com         EIN: 82-5217331

Jumapili 2:00 – 4:00                                                                    11 Oktoba 2020

Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;
nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944

4 Oktoba 2020

     

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com         EIN: 82-5217331

   KARIBU TUJIFUNZE NENO LA MUNGU KWENYE KANISA

                                                              LA

                  SWAHILI  EVANGELICAL  LILIPO GEORGIA ATLANTA.

                                                     OCT.04th  – 2020

THEME: TABIA NNE ZA KIMWILI ZA WATU WASUMBUAO KANISA LA KRISTO.

ANDIKO : WARUMI. 8:8Wale waufuatao Mwili awawezi kumpendeza Mungu”

NASABA FUPI YA KITABU CHA WARUMI:

Kwa ufupi waraka huu uliandikwa na Paulo Mtume kwa mataifa mnamo mwaka wa 57 AD, pale  Korintho, Nyaraka hii iliandikwa wakati Paulo akijiandaa kwenda Jerusalemu.

Lengo la kitabu hiki :

1. Lengo kubwa kabisa ilikuwa nikuwaonya wakristo  na Kanisa lilioko Rumi ili wawe na Imani ya kweli katika Kristo Yesu,

2. Ilikuwa ni kujitambulisha kwake, kwa wakristo walioko Rumi kabla ya yeye kufika pale Rumi.

            Tujifunze kuhusu Tabia nne za watu wanao tesa Kanisa la Kristo.

Tabia #:01. WATU WENYE ROHO YA WIVU.( Watu wa Kimwili)“Rom.8:8” “ Mwaz.3:3 ”

 Asili ya wivu ni shetani.

Tabia #:02. WATU WA  KIBURI  na MAJIVUNO (watu wakimwili) “Mith. 8:13, Luk.1:51”

Mfano: Maisha ya watu Hapa Marekani.

Tabia #: 03. Roho ya Kupenda Vyeo Visivyo kukustahili na kutotii mamlaka yaliyopo,

                                          (viongozi wa kimwili) “Roma.13:1-3”

Tabia #: 04. Watu wasio Tii Neno la Mungu. “ Rom.2:8,”

                                                                                –  Awataki Maombi,

                                                                                –  Awataki kujifunza Neno la Mungu,

                                                                                –  Watu watabia zote za dhambi.

Watu wa Tabia hizo hukumu kubwa ya kutisha inawasubiri na wote watatupwa kwenye ziwa la moto.”Ebr.10:27”.

NB: Kwaiyo inatupasa tuache tabia zote za kimwili na tumfanyiye Mungu kazi kwa Upendo, Amani, Ushirika Mtakatifu. “Yak.4:7”

Inawezekana maisha yako yako hatarini pasipo kufahamu, umetenda dhambi pasipo kujuwa lakini pia Unaishi maisha ya kulazimishwa kidhambi, Naomba uje tuombe Pamoja na wewe.

                                          Mbarikiwe Nyote na Kristo Bwana Wetu.

                                      By Pastor. Mokwa Ferdinand John.

                                                                             AMEN.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944