24 Januari 2021
Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta
“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”
www.swahilievangelical.com EIN: 82-5217331
Jumapili 3:30 – 5:30 24 Januari 2021
Kutoka 16: 2 – 9
2 Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung’unikia Musa na Haruni, huko barani;
3 wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa Bwana katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote.
4 Ndipo Bwana akamwambia Musa, Tazama, mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mkate kutoka mbinguni; na hao watu watatoka nje na kuokota kila siku sehemu ya siku; ili nipate kuwajaribu, kwamba watakwenda katika sheria yangu, ama sivyo.
5 Kisha itakuwa siku ya sita, ya kwamba watayaandaa hayo watakayoleta ndani, nayo yatakuwa ni mara mbili kuliko wayaokotayo kila siku.
6 Musa na Haruni wakawaambia wana wote wa Israeli, Jioni ndipo mtakapojua ya kuwa Bwana amewaleta kutoka nchi ya Misri;
7 na asubuhi ndipo mtakapouona utukufu wa Bwana; kwa kuwa yeye asikia manung’uniko yenu mliyomnung’unikia Bwana; na sisi tu nani, hata mkatunung’unikia?
8 Musa akasema, Ndilo litakalokuwa, hapo Bwana atakapowapa nyama wakati wa jioni mle, na asubuhi mikate hata mkakinai; kwa kuwa Bwana asikia manung’uniko yenu mliyomnung’unikia yeye; na sisi tu nani? Manung’uniko yenu hayakuwa juu yetu sisi, ila juu ya Bwana.
9 Musa akamwambia Haruni, Haya, sema na mkutano wote wa wana wa Israeli, Njoni karibu mbele ya Bwana; kwa kuwa yeye ameyasikia manung’uniko yenu.
Waefeso 4: 29
29 Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.
Warumi 1: 28 – 31
28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
Warumi 12: 2 – 3
2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.
3895 Church Street, Clarkston, GA 30021
(641) 990-7245 (404) 587-0944