9 Agosti 2020

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com         EIN: 82-5217331

Jumapili 2:00 – 4:00                                                                                                    9 Agosti 2020

1 Wakorintho 11: 23 – 26

23 Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,
24 naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.
26 Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

Luka 22: 7 – 22

Ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja pasaka.
Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie pasaka tupate kuila.
Wakamwambia, Wataka tuandae wapi?
10 Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye.
11 Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki wapi chumba cha wageni, nipate kula pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu?
12 Naye atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa; andaeni humo.
13 Wakaenda, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa pasaka.
14 Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye.
15 Akawaambia, Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu;
16 kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.
17 Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi;
18 Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja.
19 Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]
21 Walakini, tazama, mkono wake yeye anayenisaliti upo hapa pamoja nami mezani,
22 Kwa kuwa Mwana wa Adamu aenda zake kama ilivyokusudiwa; lakini, ole wake mtu yule amsalitiye!

1 Wakorintho 11: 27 – 29

27 Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.
28 Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.
29 Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944

2 Agosti 2020

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com                                  EIN: 82-5217331

 

Jumapili 2:00 – 4:00                                                                                              2 Agosti 2020

Mwanzo 2: 4 – 24

Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi
hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;
ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.
Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
10 Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne.
11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu;
12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham.
13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi.
14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati.
15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
19 Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
20 Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.
21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944

26 Julai 2020

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com           EIN: 82-5217331

Jumapili 2:00 – 4:00                                                                                                  26 Julai 2020

Matendo Ya Mitume 3: 1 – 7

Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa.
Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu.
Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka.
Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi.
Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao.
Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.
Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.

Yohana 4: 35

35 Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.

Mathayo 26: 27

27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki;

1 Wakorintho 12: 11; 14:5

12: 11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.

14: 5 Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.

Yakobo 1: 27

27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

Wagalatia 6: 1 – 5

Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.
Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake.
Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake.
Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944

19 Julai 2020

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com              EIN: 82-5217331

Jumapili 2:00 – 4:00                                                                                      21 Julai 2020

Mwanzo 1: 1 – 25

Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.
Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.
Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.
Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
10 Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.

12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
13 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.
14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;
15 tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo.
16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.
17 Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi
18 na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
19 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.

20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.
21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
22 Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.
23 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.
24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944

14 Juni 2020

Swahili Evangelical Refugee Fellowship of Atlanta

“Sisi tulio katika huduma hii ya kiuinjilisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanao abudi kwa lugha ya Kiswahili walio na shauku ya kukua katika utiifu na Imani na hamu ya kubadilisha jamii ya wakimbizi waliotuzingira.”

www.swahilievangelical.com         EIN: 82-5217331

Jumapili 2:00 – 4:00                                                                                                  14 Juni 2020

Kutoka 3: 8 – 10

nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
10 Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.

2 Wakorintho 5: 18 – 20

18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
20 Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.

2 Wakorintho 6: 1

1 Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.

3895 Church Street, Clarkston, GA 30021

(641) 990-7245             (404) 587-0944